DAMIJA MK MAKENE MICHUZI MWANDANI NDESANJO CHARAHANI AISHA ABDI MAVAZI SHAMIM MAGGID WATANZANIA Jumuia ya Wanablogu wa Tanzania
UNO AU EAC TANZANIA EU NASA REUTERS IPP Muungano wa Vijana Duniani dhini ya UKIMWI TIG IPP
NITUMIE BARUA PEPE

Rasta Model
Saturday, October 31, 2009

Rasta Model, originally uploaded by Kaka Pori.

Hapa anaonekana kaka Ridhwani mi hupenda kumwita iRasta!

Muandishi: Kaka Poli Saa: 3:33 pm | Permalink | comments: 2
Nimerudi .....!!!!!!!
Saturday, October 24, 2009
Jana katika pita pita ya mitaa ya kati nikakutana na timbwili timbwili (sio la asha ngedere) bali ni PAKA vs PANYA. Hebu fuatilia: -

Picha lilianza hivi ......


Halafu likaendelea hivi......

Likaendelea .........

Tutaendelea kesho, hilo ni trela tu!!!
Muandishi: Kaka Poli Saa: 5:49 pm | Permalink | comments: 0
kaka
Monday, December 03, 2007

kaka, originally uploaded by Kaka Pori.

Just chilling

Muandishi: Kaka Poli Saa: 12:29 pm | Permalink | comments: 2
Kwa Mapenzi Haya .....
Tuesday, June 12, 2007
Leo hii ukipita maeneo hasa ya mijini na zaidi katika sehemu za kuuzia vileo, vijiweni, maofisini majumbani na maeneo mengine yenye mikusanyiko si ajau kukuta watu wakibishana juu ya timu mbalimbali za ulaya kama vile Liverpool, Arsenal, Manchester United, Chelsea, Inter Milan, AC Milan, AS Roma, Club Bordoux, FC Monaco, Lyon FC, Marseille, n.k.



Mdau mkubwa wa globu ya picha Tanzania, mjomba Michuzi ni mmoja kati ya kundi kubwa la Watanzania wenye mapenzi ya dhati kabisa na timu za soka za Ulaya.



Bado ukitembelea maeneo hayo hayo niliyoyataja hapo juu ni dhahiri kabisa kusikia watu mbalimbali wakisikiliza muziki na hata wakati mwingine kubishana juu ya muziki hasa kutoka huko huko Ulaya na Marekani. Ukikutana na vijana 10 barabarani leo hii na ukawauliza kama wanawafahamu wanamuziki kama Jay - Z, Rihanna, Ja Rule, 50 Cent, Beyonce, n.k. kama si wote basi 8 kati yao watakwambia kuwa wanawafahamu tena kwa undani wanamuziki hao na kwa mapenzi ya dhati kabisa tuliyonayo kwao si jambo la ajabu kukuta tunavaa nguo zenye picha na nembo zao.



Mfumo wa maisha yetu kwa ujumla umeathiriwa sana tena sana na umagharibi kiasi kwamba asili yetu sasa kwa walio wengi imebaki hadithi tena hadithi ya kale. Tamaduni zetu zinabaki kuwekwa kweny majumba ya makumbusho kwa ajili ya vizazi vijavyo. Mavazi kama khanga, vitenge; tazama picha hapa chini

















Yamebaki kuvaliwa kwenye maonyesho ya mavazi na maeneo ya vijijini.



Hali hiyo hapo juu inatokana na maendeleo makubwa ya sayani na teknolojia ambapo upashanaji wa habari na taarifa umekuwa rahisi zaidi kwa kupitia magazeti, majarida, redio, runinga, n.k. Kwa kutumia utandawazi wenzetu wametuzidi ujanja kwa kuweza kupromoti sana tamaduni za kwao na kufanikiwa kutupumbaza sisi na kupelekea kusahau kabisa tamaduni zetu.

Kwa mapenzi tuliyonayo haya tukiyarudisha kwetu na kuwa na uzalendo wa kweli, tunaweza kuchukua muda mfupi sana kupiga hatua za kimaendeleo katika nyanja zote muhimu za kijamii kama vile siasa, uchumi, burudani, n.k.



Shime shime Watanganyika tufikirie upya na kutafuta njia mbadala!!!



Picha zote kwa hisani ya Michuzi
Muandishi: Kaka Poli Saa: 11:46 am | Permalink | comments: 3
Monday, March 26, 2007
MK GROUP YAZINDULIWA.

 MK Group: We always target on Perfection
MK Group Logo.

Mdau bingwa wa mitandao MK ambaye ametutengenezea blogu zetu wanablogu wengi wa kibongo hadi zikapendeza anapenda kutufahamisha ya kwamba amefungua website itakayotoa huduma za web hosting, designing na domain Registration.

unaweza kumtembelea kwa kufuata link hii http://www.mkgroupltd.com

jina la kampuni yake ni MK Group ambayo pia inajishughulisha na itajishughulisha na huduma za uuzaji wa mafuta ya Petrol, Diesel na Kerosene bongo...

kazi kwetu


Muandishi: Kaka Poli Saa: 11:43 am | Permalink | comments: 0
Nafasi ya ufadhili wa Masomo!!
Friday, November 24, 2006
Habari za leo waungwana!

Nimetumiwa barua pepe kutoka idara ya Rasilimali Watu, Sayansi na Teknolojia ya Umoja wa Afrika (UA - AU) usiku wa jana yenye kichwa cha habari: MWALIMU NYERERE AFRICAN UNION SCHOLARSHIP SCHEME INTRODUCTION. Mstari wa kifo ni tar. 30 Nov, 2006

Maelezo yote kwa kizungu haya hapa: -

DEPARTMENT OF HUMAN RESOURCES, SCIENCE AND TECHNOLOGY

MWALIMU NYERERE AFRICAN UNION SCHOLARSHIP SCHEME INTRODUCTION

The African Union has a vision of peace, integration, prosperity and peerage in the global community; an Africa led by its own people with a proud African identity; where African solutions are developed for African problems.
To achieve the vision of the African Union, engender sustainable development and meet millennium development goals, there is need to step up efforts to develop, nurture and retain a critical mass of human resources, particularly in the areas of science and technology. Support is also necessary to enhance the quality of teaching of these critical disciplines. For this reason, the African Union Commission has established the Mwalimu Nyerere African Union Scholarship Scheme.
The Mwalimu Nyerere African Union Scholarship Scheme is designed to enable African students to undertake degree programmes of study (Bachelors', Masters' and PhD) in leading African Universities, in the areas of science and technology, with a binding agreement that the beneficiaries will work in an African country for 2 to 5 years after graduation.For the first year of the Mwalimu Nyerere AU Scholarship Scheme, the African Union Commission has made provision for up to 50 scholarships at Bachelors' Degree level; all beginning in the year 2007. The next tranche will include scholarships for postgraduate studies.The Scholarship will cover all fees related to tuition and examination, return transport from home town to the University, and a modest subsistence allowance.
CRITERIA FOR SELECTION
Criteria for selection of candidates for the First Tranche are therefore as follows:
(i) Candidates:· Nationals of African Union Member States· Top performers in Member States in
science and technology related fields· Age: below 25 years for Bachelors degree· Admission to
a leading university in any African Union Member State· Must be willing to commit to work in
an African country for a minimum of 3 years after completion of studies.
(ii) Subject areas: The following fields of study will be eligible for scholarship · Engineering and
Technology (Civil, Electrical, mechanical, Chemical engineering)· B.Sc. in various fields,
including biological sciences, chemistry, astronomy, mathematics, physics, quantity surveying,
electronics, Information technology, agriculture, pharmacy
(iii) Country of StudyAny reputable African University in any African Union Member State.
Candidates are encouraged to seek admission from universities in countries other than their
own.
APPLICATION PROCEDURE
Those who meet the listed criteria are requested to apply confidently, by filling in and sending back the attached application form with copies of the following:· Relevant certificates· Letter of admission to a reputable African University· Curriculum vitae indicating age, nationality, working experience, and names and · Contacts of three referees, one of which should be from the school principal of the last school/college attended.Candidates should request referees to send reference letters directly to the AU Commission. Candidates should also explain in an essay of not more than 2,000 words, why they chose their field of study, and its importance to Africa.
Due to the expected high volume of applications, only short-listed candidates will be contacted.Send applications with supporting documents before 30th November 2006, to: -
Head of Education DivisionAfrican Union Commission
P.O. Box 3243,
Addis Ababa Ethiopia
Email nyererescheme@ africa-union. org
Tovuti: www.africa-union.org
SHIME WANAJUMUIA, KAMA HUWEZI WEWE KUNA MWINGINE ANAWEZA MPE NAFASI!!
Muandishi: Kaka Poli Saa: 9:18 am | Permalink | comments: 7
Thursday, November 16, 2006















hapa nilikuwa nikishiriki e-mkutano juu ya uundwaji wa bodi ya wakurugenzi wa YAC.

Naweka neno kidogo kwenye blogu yangu hasa nikiwa na homa ya Mkutano (ambao napenda kuuita Mkuu) wa kwanza kwa wanablogu wa Tanzania. Harakati hizi zinachangia sana katika kukuza jumuiya yetu mtandaoni (E - Community). Kwa taarifa za leo, mkutano huu utafanyika Novemba 28, 2006 majira ya saa 8 mchana kwa saa za Tanzania. Hapa ndipo nilipododosa taarifa hizo ila kwa taratibu na masuala yote yahusuyo mkutano huo ambao utawezeshwa kwa kutumia mtandao huu hapa, tembelea hapa ambapo maelezo ya kina juu ya mkutano huu yamewekwa na ukipata kukutana na kemera ya mjomba Michuzi basi ameweka maelezo pale kwa urahisi wa kufikika kwenye hicho chumba cha mkutano.

Sina pingamizi la ajenda na wala kiongozi ( kaka msangi) aliyependekezwa kuongoza mkutano huo.

Nataraji ushiriki kamilifu toka kwa wanablogu wote Watanzania katika mkutano huu adhimu. Kama kuna mtu analo azimio la dodoma, basi naomba anitumie katika anuani yangu ya barua pepe tafadhali, nataka kulipitia tena!

Tukutane Mkutanoni
Muandishi: Kaka Poli Saa: 7:27 pm | Permalink | comments: 0
Kwa Taarifa Yako!
Sunday, August 27, 2006
Tangu gonjwa la UKIMWI lilipogundulika duniani, zaidi ya watu milioni 50 katika Afrika wamekwishaambukizwa virusi vyake ambapo watu zaidi ya milioni 22 tayari wameshakufa mpaka sasa. Nchi 21 duniani zinazoongoza kwa kuwa na idadi kubwa ya watu wanaoishi na virusi vya UKIMWI zote zipo kusini mwa Jangwa la Sahara. La kutia hofu zaidi ni kwamba kati ya vijana walio katika umri wa kati ya miaka 14 – 24, asilimia 4.6 ya wanawake na asilimia 1.9 ya wanaume tayari wameshaambukizwa virusi vya UKIMWI.

Tafiti mbalimbali zinaonyesha kwamba katika idadi inayosadikiwa kufikia milioni 40 ya watu ambao tayari wameambukizwa UKIMWI duniani, nchi zinazoendelea zina zaidi ya asilimia 95 ya watu wote wanaoishi na virusi vya UKIMWI. Nchi zilizo kusini mwa Jangwa la Sahara Tanzania ikiwemo ambapo kuna zaidi ya asilimia 10 ya idadi ya watu wote duniani, eneo hilo lina zaidi ya asilimia 65 ya watu wanaoishi na virusi vya UKIMWI ambapo idadi yao hadi kufiki mwishoni mwa mwaka 2005 ilikuwa inafikia watu milioni 25.8. Katika mwaka huo huo wa 2005, idadi ya watu waliopata maambukizi mapya katika nchi zilio kusini mwa Jangwa la Sahara ilikuwa inakadiriwa kufikia milioni 3.5 ambapo idadi ya wazee, vijana, na watoto waliokufa kwa gonjwa hili ilifikia watu milioni 2.4

Pamoja na malaria, vita vya wenyewe kwa wenyewe, lishe duni, umaskini na mengineyo kadha wa kadha, UKIMWI pia ni moja kati ya wazalishaji wakubwa wa watoto yatima katika nchi zilizo kusini mwa Jangwa la Sahara ambapo idadi kubwa ya watoto ambao wazazi ama walezi wamefariki kutokana na ugonjwa huu wanalazimika kuacha shule na wengi wao kukimbilia maeneo ya mijini na kuwa wa watoto mitaani. Wanapokuwa mitaani watoto hawa hujikuta wakijiingiza katika magenge ya kihuni na kushiriki katika matumizi ya wadawa ya kulevya; biashara ya ukahaba haswa kwa wasichana; wizi na kadhalika.

Katika kufikisha ujumbe unaohusu gonjwa hili kwa jamii, njia mbalimbali zilizotumika kama vile matangazo ya redio na runinga, mabango ya barabarani, kushirikisha asasi za kiserikali na zisizo za kiserikali, watu binafsi na kadhalika zimethibitisha kwamba idadi kubwa ya watu ambapo inafikia zaidi ya asilimia 79.6 katika nchi zilizo kusini mwa Jangwa la Sahara wanafahamu juu ya ugonjwa huu kuanzia maambukizi mpaka matokeo yake.Pamoja na matokeo ya tafiti mbalimbali na takwimu zilizooredheshwa hapo juu, kadri siku zinavyozidi kusonga mbele ndivyo idadi ya watu wanaoambukizwa virusi vya UKIMWI nayo inaongezeka kwa kasi ya ajabu.

Je, umeshawahi kujiuliza tatizo liko wapi?
Muandishi: Kaka Poli Saa: 12:48 pm | Permalink | comments: 2
Yaliyojiri Juma Hili!
Wednesday, May 10, 2006
Habari za jioni wanablogu wote wa kiswahili na hata wa lugha nyingine mbalimbali duniani.

Kwanza, nachukua fursa hii adhimu kuwa shukuru wote mliotembelea blogu yangu, wale wote mlionipa pole kutokana na masahibu yaliyonikuta, basi nawashukuru sana sana. Naamini nitapona sawa sawia. Kwa taarifa tu ni kwamba, sasa hivi naendelea vizuri, jicho langu limepunguza maumivu kwa kiasi kikubwa sana, na pia bado nazidi kurudisha uoni.

Leo hii pia nina furaha kubwa sana kuwatambulisha wanablogu wawili wapya kabisa katika ulimwengu wa blogu, lakini pia ni wanaharakati madhubuti wa masuala ya haki za binadamu, haki za watu wenye ulemavu, maendeleo na mambo kadhaa chanya kwetu.

Mmoja kati ya hao wanablogu wapya ni ndugu Mkatambo, yeye ni Afisa Sheria Mkuu hapa Kituo cha msaada wa sheria Magomeni.

Mwingine ni Mtanganyika, huyu mheshimiwa naye mambo yake mjionee tu wenyewe.

Kwa kuwa bado sijawa na utaalam wa kuingiza viunga na pia kuwatangaza hawa jamaa katika blogu yangu, naamini wanablogu wenzangu wenye utaalamu huo mtalibeba jukumu hilo kwa utayari na ukamilifu wake. Hata hivyo, bado ninajitahidi kwa kasi ya ajabu katika kuupitia mwongozo wa wanablogu na miongozo mingine, basi si haba labda siku si chache na mimi nitakuwa mbali katika kujitangaza na kuwatangaza wenzangu.

Kwa J'tano ya leo, yaliyojiri ni hayo, wassalaam nawatakia juma jema.

Karibuni wanaharakati
Muandishi: Kaka Poli Saa: 7:43 pm | Permalink | comments: 0
Kimya Kingi ..............
Saturday, May 06, 2006


Amani na Uhuru wa kweli viwe nanyi nyote ndugu zangu. Naandika waraka huu nikiwakumbuka ndugu zangu ambao nimewatupa kwa muda mrefu sana hapa kwenye blogu.

Maisha ni safari, kwa maana hiyo wote tunaoishi hayo maisha basi ni wasafiri. Msemo huu ninausema ukiwa na muktadha wa kuwajulisha wenzangu juu ya mikasa iliyonikuta katika hizo harakati zangu za safari ya maisha. Najua kutokana na kutokuwa na taarifa wengi wenu mmekuwa mkijiuliza huyu Bw. mdogo vp? Mbona haeleweki!!

Kwanza, kabisa nilitingwa sana sana na masuala ya kifamilia kiasi kwamba nilikuwa nakosa kabisa muda wa kuingia mtandaoni.

Lakini pia, mnamo tarehe 2-04-2006 siku ya Jumamosi majira ya saa kumi na mbili asubuhi, nilipatwa na mkasa ambao hata sijui nisemeje. Nimetoka nyumbani maeneo ya Kinondoni B salama salimini, nikapanda daladala ya kuelekea buguruni, nikashuka kituo cha Magomeni Mikumi, nikavuka barabara, huyoo kiguu na njia naelekea ofisini kwangu pale Kituo cha Msaada wa Sheria Magomeni. Wakati nakatiza barabara ya kuingilia soko la Magomeni nyuma yangu kulikuwa na kundi la vijana karibu sita wakija pia katika uelekeo wangu, ghafla nikajikuta nimepigwa roba ya nguvu maana majamaa yalikuwa mashababi kweli kweli huku wakianza kazi ya kunisachi kama nina chochote kile kwa ajili yao, nami nikaanza harakati za kujihami, basi kilichoendelea hapo nimekuja kuhadithiwa siku ya pili. Baada ya kisanga kile ambacho kilichukuwa takriban dakika kumi hivi, nilitolewa pale eneo la tukio na raia wema na kupelekwa hadi ofisini ambapo taratibu zilifanyika na wafanyakazi wenzangu kunipeleka pale kituo cha Polisi Usalama Magomeni, ambapo nilipatiwa PF 3 na kupelekwa mwananyamala hospitali ambapo nilipewa rufaa mpaka Muhimbili, siku hiyo fahamu zilinirejelea baada ya angalau masaa sita hivi tangu alfajiri ile. Wale jamaa hawakufanikiwa kunichukulia chochote kile kati ya vitu ambavyo nilikuwa navyo mfukoni yaani simu na hela kidogo ila wameniachia jeraha litakalonikaa moyoni kwa muda mrefu kiasi. Wameniumiza sana sana jicho langu la kulia kasi kwamba kwa sasa halioni vizuri kabisa. Nimefanya X-Ray karibu sehemu zote muhimu mwilini na kukutwa niko salama jambo ambalo kwalo namshukuru sana mola.

Nimetoka hospitali siku ya J'mosi ya tarehe 29 -04-06 jioni na nimeanza kuja kazini rasmi leo J'mosi ya tarehe 06-05-06.

Lakini pia nikiwa hospitali nilitumia muda huo kutathmini ushiriki wangu kwenye kuendelea hili gurudumu la blogu na kujipanga upya katika uwasilishi wa yale yaliyo moyoni mwangu katika kujenga jamii chanya. Kwa kuanzia, nitakuwa nikiandika kwa mrengo ule ule nilioanza nao awali, pia nitakuwa nikiandika kwa juma mara moja ambapo kwa kuanzia nimeonelea siku ya J'tano kuwa ni siku muafaka kwangu kutoa muktadha ambao nitakuwa nimeukusanya kwa takriban juma lote.

Safari ya maisha bado inaendelea! Tuonane juma lijalo!!!!!
Muandishi: Kaka Poli Saa: 10:54 am | Permalink | comments: 5
eXTReMe Tracker