
hapa nilikuwa nikishiriki e-mkutano juu ya uundwaji wa bodi ya wakurugenzi wa YAC.
Naweka neno kidogo kwenye blogu yangu hasa nikiwa na homa ya Mkutano (ambao napenda kuuita Mkuu) wa kwanza kwa wanablogu wa Tanzania. Harakati hizi zinachangia sana katika kukuza jumuiya yetu mtandaoni (E - Community). Kwa taarifa za leo, mkutano huu utafanyika Novemba 28, 2006 majira ya saa 8 mchana kwa saa za Tanzania. Hapa ndipo nilipododosa taarifa hizo ila kwa taratibu na masuala yote yahusuyo mkutano huo ambao utawezeshwa kwa kutumia mtandao huu hapa, tembelea hapa ambapo maelezo ya kina juu ya mkutano huu yamewekwa na ukipata kukutana na kemera ya mjomba Michuzi basi ameweka maelezo pale kwa urahisi wa kufikika kwenye hicho chumba cha mkutano.
Sina pingamizi la ajenda na wala kiongozi ( kaka msangi) aliyependekezwa kuongoza mkutano huo.
Nataraji ushiriki kamilifu toka kwa wanablogu wote Watanzania katika mkutano huu adhimu. Kama kuna mtu analo azimio la dodoma, basi naomba anitumie katika anuani yangu ya barua pepe tafadhali, nataka kulipitia tena!
Tukutane Mkutanoni