DAMIJA MK MAKENE MICHUZI MWANDANI NDESANJO CHARAHANI AISHA ABDI MAVAZI SHAMIM MAGGID WATANZANIA Jumuia ya Wanablogu wa Tanzania
UNO AU EAC TANZANIA EU NASA REUTERS IPP Muungano wa Vijana Duniani dhini ya UKIMWI TIG IPP
NITUMIE BARUA PEPE

Kwa Taarifa Yako!
Sunday, August 27, 2006
Tangu gonjwa la UKIMWI lilipogundulika duniani, zaidi ya watu milioni 50 katika Afrika wamekwishaambukizwa virusi vyake ambapo watu zaidi ya milioni 22 tayari wameshakufa mpaka sasa. Nchi 21 duniani zinazoongoza kwa kuwa na idadi kubwa ya watu wanaoishi na virusi vya UKIMWI zote zipo kusini mwa Jangwa la Sahara. La kutia hofu zaidi ni kwamba kati ya vijana walio katika umri wa kati ya miaka 14 – 24, asilimia 4.6 ya wanawake na asilimia 1.9 ya wanaume tayari wameshaambukizwa virusi vya UKIMWI.

Tafiti mbalimbali zinaonyesha kwamba katika idadi inayosadikiwa kufikia milioni 40 ya watu ambao tayari wameambukizwa UKIMWI duniani, nchi zinazoendelea zina zaidi ya asilimia 95 ya watu wote wanaoishi na virusi vya UKIMWI. Nchi zilizo kusini mwa Jangwa la Sahara Tanzania ikiwemo ambapo kuna zaidi ya asilimia 10 ya idadi ya watu wote duniani, eneo hilo lina zaidi ya asilimia 65 ya watu wanaoishi na virusi vya UKIMWI ambapo idadi yao hadi kufiki mwishoni mwa mwaka 2005 ilikuwa inafikia watu milioni 25.8. Katika mwaka huo huo wa 2005, idadi ya watu waliopata maambukizi mapya katika nchi zilio kusini mwa Jangwa la Sahara ilikuwa inakadiriwa kufikia milioni 3.5 ambapo idadi ya wazee, vijana, na watoto waliokufa kwa gonjwa hili ilifikia watu milioni 2.4

Pamoja na malaria, vita vya wenyewe kwa wenyewe, lishe duni, umaskini na mengineyo kadha wa kadha, UKIMWI pia ni moja kati ya wazalishaji wakubwa wa watoto yatima katika nchi zilizo kusini mwa Jangwa la Sahara ambapo idadi kubwa ya watoto ambao wazazi ama walezi wamefariki kutokana na ugonjwa huu wanalazimika kuacha shule na wengi wao kukimbilia maeneo ya mijini na kuwa wa watoto mitaani. Wanapokuwa mitaani watoto hawa hujikuta wakijiingiza katika magenge ya kihuni na kushiriki katika matumizi ya wadawa ya kulevya; biashara ya ukahaba haswa kwa wasichana; wizi na kadhalika.

Katika kufikisha ujumbe unaohusu gonjwa hili kwa jamii, njia mbalimbali zilizotumika kama vile matangazo ya redio na runinga, mabango ya barabarani, kushirikisha asasi za kiserikali na zisizo za kiserikali, watu binafsi na kadhalika zimethibitisha kwamba idadi kubwa ya watu ambapo inafikia zaidi ya asilimia 79.6 katika nchi zilizo kusini mwa Jangwa la Sahara wanafahamu juu ya ugonjwa huu kuanzia maambukizi mpaka matokeo yake.Pamoja na matokeo ya tafiti mbalimbali na takwimu zilizooredheshwa hapo juu, kadri siku zinavyozidi kusonga mbele ndivyo idadi ya watu wanaoambukizwa virusi vya UKIMWI nayo inaongezeka kwa kasi ya ajabu.

Je, umeshawahi kujiuliza tatizo liko wapi?
eXTReMe Tracker