DAMIJA MK MAKENE MICHUZI MWANDANI NDESANJO CHARAHANI AISHA ABDI MAVAZI SHAMIM MAGGID WATANZANIA Jumuia ya Wanablogu wa Tanzania
UNO AU EAC TANZANIA EU NASA REUTERS IPP Muungano wa Vijana Duniani dhini ya UKIMWI TIG IPP
NITUMIE BARUA PEPE

Kwa Mapenzi Haya .....
Tuesday, June 12, 2007
Leo hii ukipita maeneo hasa ya mijini na zaidi katika sehemu za kuuzia vileo, vijiweni, maofisini majumbani na maeneo mengine yenye mikusanyiko si ajau kukuta watu wakibishana juu ya timu mbalimbali za ulaya kama vile Liverpool, Arsenal, Manchester United, Chelsea, Inter Milan, AC Milan, AS Roma, Club Bordoux, FC Monaco, Lyon FC, Marseille, n.k.Mdau mkubwa wa globu ya picha Tanzania, mjomba Michuzi ni mmoja kati ya kundi kubwa la Watanzania wenye mapenzi ya dhati kabisa na timu za soka za Ulaya.Bado ukitembelea maeneo hayo hayo niliyoyataja hapo juu ni dhahiri kabisa kusikia watu mbalimbali wakisikiliza muziki na hata wakati mwingine kubishana juu ya muziki hasa kutoka huko huko Ulaya na Marekani. Ukikutana na vijana 10 barabarani leo hii na ukawauliza kama wanawafahamu wanamuziki kama Jay - Z, Rihanna, Ja Rule, 50 Cent, Beyonce, n.k. kama si wote basi 8 kati yao watakwambia kuwa wanawafahamu tena kwa undani wanamuziki hao na kwa mapenzi ya dhati kabisa tuliyonayo kwao si jambo la ajabu kukuta tunavaa nguo zenye picha na nembo zao.Mfumo wa maisha yetu kwa ujumla umeathiriwa sana tena sana na umagharibi kiasi kwamba asili yetu sasa kwa walio wengi imebaki hadithi tena hadithi ya kale. Tamaduni zetu zinabaki kuwekwa kweny majumba ya makumbusho kwa ajili ya vizazi vijavyo. Mavazi kama khanga, vitenge; tazama picha hapa chini

Yamebaki kuvaliwa kwenye maonyesho ya mavazi na maeneo ya vijijini.Hali hiyo hapo juu inatokana na maendeleo makubwa ya sayani na teknolojia ambapo upashanaji wa habari na taarifa umekuwa rahisi zaidi kwa kupitia magazeti, majarida, redio, runinga, n.k. Kwa kutumia utandawazi wenzetu wametuzidi ujanja kwa kuweza kupromoti sana tamaduni za kwao na kufanikiwa kutupumbaza sisi na kupelekea kusahau kabisa tamaduni zetu.

Kwa mapenzi tuliyonayo haya tukiyarudisha kwetu na kuwa na uzalendo wa kweli, tunaweza kuchukua muda mfupi sana kupiga hatua za kimaendeleo katika nyanja zote muhimu za kijamii kama vile siasa, uchumi, burudani, n.k.Shime shime Watanganyika tufikirie upya na kutafuta njia mbadala!!!Picha zote kwa hisani ya Michuzi
Muandishi: Kaka Poli Saa: 11:46 am | Permalink |


2 Comments:


 • Saa: Monday, November 26, 2007 2:37:00 pm, Mtoa Maoni: Blogger EDWIN NDAKI

  kaka unayoyasema ni ya kweli kabisa.

  Mbali na mavazi pia ukiangalia sanaa zetu nyingi za maonyesho mfono ngoma za utamaduni.

  Leo hii utakutana nazo pale EYA POTI wakati wakupokea wageni..na zaidi ya hap labda uende kwenye tamasha la Bagamoyo au kwenye shughuli za serikali mara chache..

  Shime kweli tusirudi kwa kasi utumwani hata kama tumeamua kurudi spidi hii inatisha.

  Ni hayo tu nawasilisha  
 • Saa: Sunday, June 14, 2015 1:18:00 am, Mtoa Maoni: Anonymous Obat Vimax

  Thanks for sharing, nice blog and article  
eXTReMe Tracker