DAMIJA MK MAKENE MICHUZI MWANDANI NDESANJO CHARAHANI AISHA ABDI MAVAZI SHAMIM MAGGID WATANZANIA Jumuia ya Wanablogu wa Tanzania
UNO AU EAC TANZANIA EU NASA REUTERS IPP Muungano wa Vijana Duniani dhini ya UKIMWI TIG IPP
NITUMIE BARUA PEPE

Nipo Wenzangu!
Tuesday, January 17, 2006
Kwanza natoa pole kwa familia za mahujaji zaidi ya 345 ambao wamefariki huko Maka katika harakati za 'kumpiga mawe shetani' ikiwa ni sehemu ya ibada 'tukufu' ya Hijja. Pia natoa pole (kwa maana kazi ilikuwa ngumu) na hongera (kwa maana imekamilika) kwa Mh. Rais Kikwete kutangaza baraza lake la mawaziri na manaibu waziri ambao idadi yao jumla ni 60, japo Wadanganyika wengi tumekubali kwa 'shingo upande' ukubwa wa baraza hilo, lakini mpangilio wa wizara na uteuzi wenyewe jinsi ulivyofanyika kama vile kupanguliwa, kuongezwa na 'kwa wanawake kupewa wizara nyeti' kwa kiasi fulani umeonyesha dira ya taifa letu kwa miaka mitano ijayo ya utwawala huu.

Kaka Macha amenikumbusha juzi kwa barua pepe juu ya ukimya wangu katika blogu. Ahsante kwa kunikumbusha japo sikuwa nimesahau hata kidogo juu ya mchango wangu bloguni. Nimepitia maandiko ya Tupende Urembo Asili ambayo Chemi ameiandika na kuchangiwa na wanablogu kadhaa kama vile Boniface Makene ambaye ripoti yake ya mwezi imenisisimua mno.

Nilitumia muda mrefu kupitia kurunzi la Msaki na uchambuzi wa hotuba ya Mh. kikwete. Nimetumia fursa hiyo pia kusoma maandiko ya ndugu yangu Reginald Miruko. Duh! Kaka Msangi ama kweli wewe ni mwanaharakati, maandiko yako yana ishara kadhaa. Mashairi ya Mkwinda pamoja na washairi wengine bloguni yamenivutia sana, hongera kwa ushairi mzuri ambao ninaamini ni moja ya nguzo kuu za kukikuza Kiswahili. Harakati za ndugu yangu Nyembo nazo ni za mfano wa kuigwa.

Bwaya ndugu yangu, uliyoyaandika wewe, wanablogu wote pamoja na kauli mbiu ya blogu yangu (soma aya tatu za mwisho), ndio haswa tunachotakiwa kufanya ili kubadilisha kizazi hiki.

Pia naomba niweke andiko hili hapa juu ya mustakbali , kwa wakati huu bado tunaendelea na tafsiri ya nyaraka mbalimbali kwa Kiswahili.

Leo wanablogu wenzangu nawatonya; mwenzenu mimi ni mfanyakazi wa kujitolea katika Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu na juma hili ndio tumeanza mwaka rasmi baada ya mapumziko ya kirismasi na mwaka mpya, hivyo nipo katika harakati za kuweka mambo sawa hapa kituoni kwetu 'Kituo cha Msaada wa Sheria Magomeni' na nitakapo kaa sawa tu, nitaandika kuhusu andiko la Chemi juu ya Urembo na Uafrika. Nimevutiwa sana na mjadala huo kwa sababu hiyo ni moja sehemu tuliyoshikiwa akili na hao wembamba wa ulaya wanaotaka na sisi tuwe kama wao kwa kila hali na kila kitu.

Amani ya Kweli na Iwe Kwenu Nyote!!
Muandishi: Kaka Poli Saa: 5:48 pm | Permalink |


2 Comments:


eXTReMe Tracker