DAMIJA MK MAKENE MICHUZI MWANDANI NDESANJO CHARAHANI AISHA ABDI MAVAZI SHAMIM MAGGID WATANZANIA Jumuia ya Wanablogu wa Tanzania
UNO AU EAC TANZANIA EU NASA REUTERS IPP Muungano wa Vijana Duniani dhini ya UKIMWI TIG IPP
NITUMIE BARUA PEPE

Mwana Mpotevu
Tuesday, March 28, 2006
Salam kwa wote. Naamini muwazima wote wa afya tele. Ni muda mrefu saaaana mwenzenu nipo nje kabisa ya ulingo wa blogu. Kuna sababu za kiufundi na za kiteknolojia pia ambazo kwa namna moja au nyingine zimenikwaza. Kwanza, kwa muda mrefu kiasi, nimekuwa nikisafiri kwenda vijijini kabisa katka harakati za kufikisha ujumbe wa haki za binadam na harakati za maendeleo, na kama mjuavyo, maeneo mengi sana ya vijijini nchini kwetu hayajafikiwa na nishati ya umeme sembuse huduma za tarakilishi na intaneti yake. Sina muda mfupi sana tangu nirudi kutokahuko na kukuta nina barua pepe nyingi sana za kujibu na kuzisoma pia. Kaka Makene, nimesoma mail na changamoto yako, sasa nakwambia nimerudi. Nimepitia blog ya macha, safi sana kaka, hizo ni harakati kombozi.

Kwa taarifa yenu, leo kuna taarifa imeandikwa magazetini juu ya Wabunge wa bunge la Tanzania kuchanga kiasi shilingi 40,000/- kwa ajili ya baa la njaa linalowakiabili ndugu zetu vijijini.
Muandishi: Kaka Poli Saa: 2:37 pm | Permalink |


3 Comments:


eXTReMe Tracker