DAMIJA MK MAKENE MICHUZI MWANDANI NDESANJO CHARAHANI AISHA ABDI MAVAZI SHAMIM MAGGID WATANZANIA Jumuia ya Wanablogu wa Tanzania
UNO AU EAC TANZANIA EU NASA REUTERS IPP Muungano wa Vijana Duniani dhini ya UKIMWI TIG IPP
NITUMIE BARUA PEPE

Ujumbe Wangu
Friday, January 27, 2006
Lile shindano la kumtafuta mlimbwende wa utalii ndo linaelekea elekea kushika hatamu sasa bila shaka ikiwa tu 'halitaghairishwa kama ilivyo ada', basi litafanyika Februari 25, 2006 pale katika hoteli ya Ngurdoto mkoani Arusha. Mwaka jana Bi. Nancy Sumari naye aliamsha shangwe za Wadanganyika kwa kuvishwa taji 'la kizushi' la Miss World Afrika kutoka Miss World. Lakini je? hivi ni kweli kuna usawa katika kuandaa mashindano haya na kumpata mrembo wa dunia? Hilo swali mimi, naamini na watu wengine wengi bado tunajiuliza. Jamani shindano la urembo wa dunia na hata hilo la mrembo wa utalii na utitiri wa mashindano ya namna hiyo, bado hayana sura ya kweli ya kumpata binti mrembo wa dunia hata kidogo. Binti wa Kiafrika ambaye Chemi anatunyambulia hapa 'ni tofauti sana na binti wa kutoka bara lingine' kimaumbile na kimuonekano. Sasa katika hali kama hii unampataje mrembo wa dunia?
Natoa changamoto ya kuanzisha vuguvugu la kutaka usawa katika masuala yote yanayogusa jamii zetu kimataifa. Kwanza tuanzie na hili la urembo ambalo Bi. Chemi Che Mponda amelirudisha katika fikra zangu. Kwa mtazamo wangu ni vigumu sana kumpata mrembo mmoja wa dunia. Kwa sababu huyo mwanamke wa Kihaya ambaye atakuwa mnene, aliyesuka kipilipili, mwenye rangi yake halisi kabisa awe ni mweusi au mweupe atakayevaa vazi la Kihaya aende akashindane na binti kutoka uingereza ambaye ni mwembamba, mrefu, mwenye nywele zilizowekwa madawa na mabinti kutoka Asia, Amerika na mabara mengine kwa pamoja washindanishwe kumpata huyo mrembo mmoja akakubalika mbele ya majaji na watazamaji hayupo.
Jamani naomba niwe muwazi kabisa kwa hili nitakalolisema hapa. Wazungu na waarabu wamefanikiwa kwa asilimia zaidi mia moja kuwafanya waafrika waone kila kile ambacho ni chao basi ni cha kishenzi na hawastahili kuwa nacho hata kidogo, na vile vya kwao ni bora. Hebu wewe unayesoma hapa sasa hivi, jiulize kuhusu jina lako, hizo nguo ulizovaa, muziki unaopenda kusikiliza, hata vipindi vya luninga unavyopenda kuvitazama, na mambo kadhaa wa kadhaa, je unaweza usema unaringia Uafrika wako?. Juzi juzi hapa wakati mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano 'wenye utata' wa Tanzania ndugu Kikwete wakati anawaapisha mawaziri katika baraza lake la Mawaziri hakuna ambaye nimemuona akiwa amevaa hilo linalopigiwa chapuo kuwa ni vazi la taifa. Ila tunaambiwa kuna vazi la Taifa ambalo Michuzi alimbamba Mwanamuziki Stara Thomas akikatisha mitaani na moja ya mitindo yake. Hata Waziri mwenye dhamana ya kuulinda Utamaduni jamani???!!! Pia ninaomba tafsiri halali ya Ibara ya 14 (g) ya Sheria ya Mwenendo wa Mashtaka ya Jinai ya mwaka 1985 kama ilivyokuwa ikirekebishwa. Ibara hiyo inasomeka hivi;
14. A police officer may without warrant arrest ..................
(g) any person who does any act which is calculated to insult the national
emblem or the national flag;
Mtanisamehe kwa 'kimombo' sheria zetu hazisomwi na Wazigua, Wachaga, Wazaramo, Wamakonde na makabila mengine ila zinasomwa na Makaka na Madada Wasomi 'the Learned Brothers and Sisters' ndio maana mpaka leo zipo katika lugha hiyo. Sina hakika pia kama kuna mkakati wa kuzitafsiri pia.
Kusema ukweli na yakini kabisa tunahitaji mapinduzi ya kimtazamo na kifikra kwani sisi ni sisi na hatuwezi kuwa wao kwa sababu hata wao hawawezi kuwa sisi kamwe.
Mjadala wa kupata neno blogu kwa kiswahili naona unazidi kupaa angani kwani wachangiaji naona wanabunga bongo kwelikweli tukazi uzi jamani ipo siku tuatalipata hilo neno tu.
Muandishi: Kaka Poli Saa: 5:43 pm | Permalink |


0 Comments:


eXTReMe Tracker