DAMIJA MK MAKENE MICHUZI MWANDANI NDESANJO CHARAHANI AISHA ABDI MAVAZI SHAMIM MAGGID WATANZANIA Jumuia ya Wanablogu wa Tanzania
UNO AU EAC TANZANIA EU NASA REUTERS IPP Muungano wa Vijana Duniani dhini ya UKIMWI TIG IPP
NITUMIE BARUA PEPE

Utatu Umetimia!!
Thursday, December 29, 2005
Hatimaye jina la Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania chini ya utawala wa awamu ya nne ya uongozi chini ya Rais Jakaya Mrisho Kikwete limewekwa wazi na kupitishwa kwa kura 212 na Bunge leo tarehe 29 Disemba, 2005 naye si mwingine bali ni aliyekuwa waziri wa Maji na Mifugo ndugu Edward Lowassa. Hiyo ni moja katika hatua mbalimbali za kuusimika uongozi wa nchi ambapo jana ndugu Samwel Sitta, waziri wa zamani wa Sheria na Katiba alipitishwa kwa kura nyingi mno kuwa Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Ambapo leo hii Bi Anna Makinda alipitishwa kuwa Naibu Spika. Bila ya shaka ukiacha kazi ya kuchagua kamati mbalimbali za Bunge itifaki chache sana zitakuwa zimebaki katika ukamilisho wake. Akitoa shukrani mara tu baada ya kuaribishwa rasmi katika kiti cha uspika alitoa nasaha ambayo imenifanyaq binafsi nikae na kufikiria kusema haya na wenzangu katika blogu (bila shaka mdahalo wa neno mbadala la blogu halijapatikana). Mheshimiwa Sitta alitoa kauli zenye kuonyesha kwa kiasi amekomaa katika siasa za nchi hii. Aliwakumbusha Wabunge wakati huo akiwa kule mkoani Kilimanjaro namna alivyokuwa mzee wa Speed and Standard akimaanisha Kiwango na Kasi kauli ambayo iliamsha shangwe bungeni. Akiongozea katika hotuba yake hiyo fupi, aliwaomba Wabunge pamoja na Mawaziri wasitoe majibu ambayo hayana utatuzi kwa matatizo halisi ya wananchi na kusisitiza kuwa Wabunge waache mzaha Bungeni.
Kauli hiyo ya Mhe. Spika imenifanya nijiulize mara kwa mara, hivi wabunge wetu kweli watarudi majimboni kuyatafutia majibu yenye utatuzi mahitaji yetu?, je? ataelewa kweli kilio cha ndugu yangu Makene juu ya mke wake Mama Masha na wakesha hoi kibao huku jimboni? Kwanza huyu mbunge wetu hakai huku jimboni kwake, miaka nenda rudi yeye anaishi huko anakoishi akiwa na miradi yake yoote huko pamoja na familia yake, nilikuwa nikimuona huku jimboni wakati uchaguzi unapokaribia karibia. na kwa katika uchaguzi huu, mara ya kwa kumuona ni kipindi kilee cha kura ya maoni ya kumpata mgombea ubunge na udiwani ambapo baada ya kutoa takrima alipitishwa, ya pili ni pale kampeni ilipoanza rasmi ambapo sasa alitoa takrima kwa wadanganyika pale jimboni hapa aligawa peremende 'hata babuyangu alipata japo kibogoyo, fulana, kofia, beji vitenge na kanga 'bibi yangu aliambulia na kuvua lile kaniki lake lililochanika', vyote hivi vikiwa na sura yake na ya mgombea urais wa chama chake, ya tatu hata sikumbuki vizuri ilikuwa wapi ila ya mwisho ni siku ile alipotambulishwa rasmi na mheshimiwa mgombea urais wa chama chake, na juzi nilimuona kupitia katika runinga kule Dodoma 'Makao Makuu ya kufoji' bungeni wakati anaapishwa ili atukimbie rasmi jimboni, na mara chache kuoneka vikaoni bungeni na kurudisha mtaji wake aliouwekeza kwa wampa kula wakati wa kampeni. Huku jimboni kwake inawezekana kabisa kwamba igizo ndio limeisha limeisha mpaka baada ya miaka mitano yaani 2010?
Muandishi: Kaka Poli Saa: 6:59 pm | Permalink |


1 Comments:


  • Saa: Monday, January 02, 2006 11:55:00 am, Mtoa Maoni: Blogger mark msaki

    Kaka pori tuombe mungu.

    sina wasi wasi sana na hiyo top brass, nilivyoisikia hotuba ya muheshimiwa raisi na jinsi ninavyowafahamu hawa wengine kwa upeo wangu mdogo ninaona kuna nia ya dhati kabisa kuibadilisha status ya tanzania kutoka kuwa kanisa hadi nchi huru!

    cheers  
eXTReMe Tracker