DAMIJA MK MAKENE MICHUZI MWANDANI NDESANJO CHARAHANI AISHA ABDI MAVAZI SHAMIM MAGGID WATANZANIA Jumuia ya Wanablogu wa Tanzania
UNO AU EAC TANZANIA EU NASA REUTERS IPP Muungano wa Vijana Duniani dhini ya UKIMWI TIG IPP
NITUMIE BARUA PEPE

Nimetandaa!!
Tuesday, December 27, 2005
"Tupo katika wakati mgumu sana katika historia ya Ulimwengu, wakati ambapo utu lazima uchague mustakbali wake. Kadri dunia inavyokuwa inategemeana na nyepesi, mustakbali nao mara moja unakuwa hatarini. Ili tuweze kujongea mbele, ni lazima tujiunge pamoja ili kuleta jamii endelevu duniani ambayo inaundwa kutokana na kuheshimu uhalisia, haki za binadamu, haki ya kiuchumi na kuwa na utamaduni wa amani. "
"Hakuna ambaye amezaliwa akiwa ni raia mwema, hakuna taifa lililozaliwa likiwa tayari na demokrasia. Zaidi, yote hiyo ni michakato ambayo inaendelea kujitokeza katika maisha yetu. Vijana lazima wajumuishwe tangu wanapozaliwa. Jamii inayojiondoa kwa vijana wake, basi itajiuguza muda wote."
Hapo juu, nimenukuu sehemu za hotuba ya Mtumishi Mkuu wa Umoja wa Mataifa Bw. Kofi Annan, aliyoitoa katika Mkutano wa Dunia wa Mawaziri wanowajibika kwa Vijana. Maneno katika hotuba za hawa viongozi wetu ni za kutia hamasa sana, kiasi kwamba vijana tumekuwa ni watu wa kuishi kwa matumaini miaka nenda rudi.
Mimi ni mwancahama wa MRADI MAALUM wa MUONGO WA Umoja wa Mataifa wa, Elimu kwa Maendeleo Endelevu 2005-2014 gonga hapa nimeshiriki katika mradi baada ya kupata mwaliko kutoka kwa rafiki yangu aliyeko Ujerumani ambaye ndiye miongoni mwa watu wa mwanzo kabisa kushiriki katika mradi huu. Moja kati ya shawishi kubwa nilizozifanya katika mradi huu ni kuhamasisha matumizi ya lugha mbalimbali ili uonekane kweli ni wa kimataifa na kuwafikia walengwa kwa lugha wanayoielewa wao kwa urahisi zaidi na pia kuwahamasisha vijana wajiunge pia. Kwa hakika nimefanikiwa katika kushawishi matumizi ya lugha mbalimbali, lakini kwa vijana kujiunga sijapata majibu ya kuridhisha kwa hilo! na kwa sasa mimi pamoja na baadhi ya vijana wenzangu kutoka Afrika Mashariki tuna jukumu la kutafsiri nyaraka za mtandao huo kwa lugha ya kiswahili tukiwa kama sehemu ya timu ya wanaojitolea katika mradi huu gonga hapa na ukishawishika jiunge tafadhali. Mimi pia ni mwanachama wa mtandao wa vijana wa taking it global gonga hapa usome habari zake.
Katika mitandao yote hii, na mingine kadha wa kadha utaona ushiriki wa vijana wa kiafrika ni mdogo ama haupo kabisa. Nakubaliana na wengi kwamba moja kati ya vikwazo katika ushiriki wetu ni ukosefu wa taarifa, hata hivyo pia zile ambazo tunazipata ni taarifa ambazo si sahihi na mara nyingi zinakuja zikiwa tayari zimeshachelewa mno.
Nashawishika kutoa hamasa kubwa kwe vijana wenzangu, jamani tusilalamike tuu, sisi wenyewe tuna utatuzi .
Muandishi: Kaka Poli Saa: 8:38 pm | Permalink |


2 Comments:


  • Saa: Friday, December 30, 2005 10:12:00 am, Mtoa Maoni: Blogger FOSEWERD Initiatives

    kaka Pori,

    nakubaliana na wewe kabisa kuwa nyakati zimebadilika. na sisi kama wananchi wa Tanzania (katika afrika tanzania ndio wazito zaidi, na hii ni kutokana na mfumo uliokuwepo kwa siku nyingi)tumekuwa wazito kujichanganya. sio hilo tu, kuna rafiki yangu alinieleza kuwa kuna nafasi nyingi za masomo huwa zinatafutra watu kutoka nchini kwetu lakini watu hawaombi inabidi wapewe waarabu. amini usiamini kukaa kwenye mtandao walau saa moja kwa siku sasa hakuepukiki.

    huo mradi mie nimeupenda. ila sasa nimebanwa na mlango kimasomo. kashesehe likishuka kidogo ninaingiza timu!

    cheers  
  • Saa: Friday, December 30, 2005 10:14:00 am, Mtoa Maoni: Blogger FOSEWERD Initiatives

    nilicheka unajua watanzania husubiri ziletwe ubalozini halafu wizarani ndio waombe. ndio maana waheshimiwa wanazichukua juu kwa juu kwa ajili ya watoto wao waliobaki wanalalamika!

    tunatakiwa pia kupunguza utegemezi kwa serekali sasa. na ndio njia moja ya msingi sana kujenga jammi huru iliya sawa na haki hata kuamua hatima yake kimaisha na kisiasa! -  
eXTReMe Tracker