DAMIJA MK MAKENE MICHUZI MWANDANI NDESANJO CHARAHANI AISHA ABDI MAVAZI SHAMIM MAGGID WATANZANIA Jumuia ya Wanablogu wa Tanzania
UNO AU EAC TANZANIA EU NASA REUTERS IPP Muungano wa Vijana Duniani dhini ya UKIMWI TIG IPP
NITUMIE BARUA PEPE

Mpo?!!
Saturday, December 31, 2005
Mwanaharakati mwenzetu ametuaga kwa kusema kwamba hatokuwepo nasi kwa takriban mwezi mzima hivi! Duh! Kwa heri lakini sio mbaya hata siku moja moja ukishuka dimbani na kutupa salamu tu!

Haya ni majibu yangu ya chemsha bongo kuhusu Afrika ambayo nimeichomoa leo kutoka kwa Ndesanjo, sijagezea kaka!!. Hii ni changamoto kweli kweli juu ya uelewa wetu kuhusu bara letu Afrika kwani asilimia nilizozipata huko zinaonyesha ni kwa kiasi gani tunatakiwa kufanya jitihada za hali ya juu kuifahamu Afrika na kila kinachoihusu. Nimeifanya hata ile chemsha bongo ya kujaza ramani ya Afrika lakini nimeifanya kuanzia ile nyepesi kabisa mpaka ile ngumu kiasi, Duh!.

Ndesanjo amesisitiza tuweke picha kwenye blogu zetu, naweka hii hapa!Hii ilikuwa mwaka 2004 katika Mkutano wa wadau wa uchaguzi kutoka katika makundi mbalimbali ya kijamii. Mimi 'niliyesimama' na Fredrick Mkatambo hapa kushoto kwangu tuliwakilisha kundi la watu wenye ulemavu kupitia Kituo cha Habari juu ya Ulemavu ICD. UNDP Dar es Salaam.


Mjadala kuhusu neno blogu kwa Kiswahili sijui umeishia wapi? Wakati huo huo nafanya jitihada za dhati kuipata hotuba ya Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Jakaya kikwete alipolihutubia bunge jana.
Muandishi: Kaka Poli Saa: 12:56 pm | Permalink |


3 Comments:


 • Saa: Sunday, January 01, 2006 2:00:00 am, Mtoa Maoni: Blogger Mija Shija Sayi

  ..Tupo, Kaka Pori mjadala wa neno blogu kwa kiswahili unaendelea hapa http://www.quicktopic.com/31/H/KOFGe3iwuy5Aq

  Ingekuwa vizuri kama kiungo hiki ukakiweka katika blogu yako, ukitembelea kwenye blogu yangu utakuta nimekiweka upande wa kulia baada ya kitabu cha picha na nimekiita "Bunga bongo ya neno blogu kwa kiswahili.

  Haya kazi kwako kaka.  
 • Saa: Sunday, January 01, 2006 10:43:00 am, Mtoa Maoni: Blogger Ndesanjo Macha

  Umeingia kwa nguvu kweli! Mjadala kuhusu neno muafaka la blogu nenda hapa: http://www.quicktopic.com/31/H/KDFGe3iwuy5Aq  
 • Saa: Sunday, January 01, 2006 10:44:00 am, Mtoa Maoni: Blogger Ndesanjo Macha

  Umeingia kwa nguvu kweli! Mjadala kuhusu neno muafaka la blogu nenda hapa: http://www.quicktopic.com/31/H/KDFGe3iwuy5Aq  
eXTReMe Tracker