DAMIJA MK MAKENE MICHUZI MWANDANI NDESANJO CHARAHANI AISHA ABDI MAVAZI SHAMIM MAGGID WATANZANIA Jumuia ya Wanablogu wa Tanzania
UNO AU EAC TANZANIA EU NASA REUTERS IPP Muungano wa Vijana Duniani dhini ya UKIMWI TIG IPP
NITUMIE BARUA PEPE

KABLA HATUJAKARIBIA UKAMILIFU WA DAHARI .....
Tuesday, December 27, 2005
Hakika leo ni siku njema sana kwangu. Nina furaha isiyo kifani kupata makaribisho mazuri kutoka kwa wanablogu wa Kiswahili. Kaka Macha! mimi pia nilikuwa mvivu katika kujifunza hesabu shuleni, lakini nimemuelewa na kumkubali ndugu Mija kwa hesabu zake "Habari chanya + Jamii hasi = Jamii chanya. Ahsante kwa chagizo hilo na nimeliweka katika akili yangu ili niweze kuliandikia. Nimekaribia kweli kweli ndugu fikrathabiti, mark msaki, egidio, mwandani, na wanablogu wote!!
Jamii ya Watanzania, hata Afrika kwa ujumla wake, tumepoteza mapenzi ya dhati na nchi zetu. Machache sana kwa leo nitayatolea mfano, pia ninaamini yameshasemwa sana; Kuna ule wimbo wa "Tanzania...Tanzania... Nakupenda kwa moyo wote........." maneno ya ule wimbo yanakaririka na kuimbika kwa ustadi mkubwa sana, nakumbuka mara ya mwisho ule wimbo kuimbwa katika mashule yetu ni miaka ya tisini kipindi kile mimi namalizia shule ya msingi. Leo hii ukikutana na vijana 10 tu wa Kitanzania na ukawaomba wakuimbie japo beti mbili tu za wimbo huo mzuri, labda 3 kati yao wataweza kukuimbia maneno yale matano ya mwanzo na yaliyobaki yatamun'gunywa mpaka uchoke mwenyewe. Lakini leo hii, kijana unayemuona ni lazima atakwambia anajua karibu nyimbo zote katika albamu la senti hamsini yule jamaa mhuni wa kule kwa joji kichaka. Hayo ndio tuliyonayo kwenye jamii yetu sasa hivi, ama kweli hiki ni kizazi kipya na cha ajabu!!
Nipo pamoja na wale wote ambao wanautukuza tamaduni zao. Hapa nina maanisha matumizi ya lugha ikiwa ndio moja ya nguzo kuu za utamaduni. Leo hii, tuna aina ya muziki ambayo imeshika hatamu katika afrika ya mashariki, na kwa hapa Tanzania inafahamika sana kama bongo flava, kadiri siku zinavyozidi songa mbele, wanaibuka waimbaji wapya, hata hivyo tangu nianze kuusikiliza muziki huu, naona bado hatujapata wawakilishi wa kutosha katika kututambulisha. Angalia mavazi yao, midundo ya nyimbo zao, hata lugha pia, halafu malizia na ujumbe katika hizo nyimbo ndio balaa!! Hapa mimi nina chagizo naliweka; tunataka Habari chanya + Jamii hasi = Jamii chanya. Tunafanya kuwaamsha hawa mambumbu wanaokebehi tamaduni zetu?
Bado tuna kazi kubwa ya kuweka wazi uzalendo wetu kivitendo kabla ya ukamilifu wa dhari maana hata bado hatujaukaribia.
Bado ninatafakri juu ya neno blogu kwa lugha yetu, nitakapolipata nitaliweka hadharani.
Mapambano yanaendelea
Muandishi: Kaka Poli Saa: 2:45 pm | Permalink |


1 Comments:


  • Saa: Friday, December 30, 2005 10:01:00 am, Mtoa Maoni: Blogger FOSEWERD Initiatives

    kaka pori!

    mimi huwaga ninafikiria. ni nini hasa kitu kinachofanya uzalendo upotee?? ni kwa nini ni kaka ben peke yake anayeweza kuuimba kwa umahiri zaidi? ukinitembelea kuna makala yangu ya awali kabisa "barua kwa raisi mpya..." imeandika sababu!

    ule wimbo huimbwa na mtu yeyote aliyekula mema ya nchi! aliyejibidiisha akaungwa mkono, aliyeheshimiwa utu wake, anayeongozwa na kiongozi anayempenda, anayeugua anapata matibabu, anayechumbia na kuweza kuweka kijiwe cha nguvu kidoleni kwa mahabuba wake! asiyelazimishwa kuishi nje ya nchi yake kama mkimbizi, anayechangia maendeleo na kuthaminiwa!

    tufanyaje sasa kurudisha uzalendo?  
eXTReMe Tracker